24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mbarawa amtaka mkandarasi kuongeza kasi mradi wa BRT 3

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Profesa Makame Mbarawa ameagiza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuhakikisha mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT 3) kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la Mboto unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati.

Prof. Mbarawa ametoa agizlo hilo mapema leo Agosti 7, jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika mradi huo wenye urefu wa zaidi ya kilomita 23.3 pamoja na vituo vya abiria aliambatana na viongozi mbalimbali ambapo amempongeza mkandarasi anayejenga mradi huo kwa kasi anayoenda nayo licha ya kuchelewa kidogo.

“Barabara hii ni muhimu na vituo vyake, mkandarasi anachelewa katika kipindi cha ujenzi, nniwaombe wakazi wa Dar es Salaam kuangazia usalama wa barabara wakati wa ujenzi hasa wakati wa mchana wawe wavumilivu katika kipindi hiki,” amesema Prof. Mbarawa.

Naye Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Frank Mbilinyi amesema mradi umechelewa kwa asilimia 2 na kwamba shughuli za ujenzi zinaendelea kufanyika kwa haraka mchana na usiku huku akiahidi kwamba utakamilika kwa muda uliopangwa kutokana na umuhimu wa barabra hiyo kwa wananchi.

“Hadi kukamilika kwa mradi huu wenye urefu wa kilomet 23.3 unatarajia kugharimu Sh bilioni 231 pamoja na vituo mbalimbali vya abiria unatarajia kuamilika mwakani ikiwemo juhudi ya Serikali kuendeleza huduma ya usafiri,” amesema Mhandisi Mbilinyi.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Nicodemas Tambo amesema barabara hiyo inawatumiaji wengi hivyo wamesisitiza ikamilike kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero.

Kwa upande wake Katibu Tawala Ilala, Chilangwa Seleman amewaomba wakandarasi kuongeza kasi barabara ikamilike kwa haraka kwasababu inategemewa na watu wengi.

Prof. Mbarawa yuko jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miundombinu mbalimbali hususani ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka BRT.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles