23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

POMBE ZA VIROBA ZAITWA CHAPATI, KICHWA

Na IBRAHIM YASSIN – KYELA


WAUZAJI na wamiliki wa maduka ya vileo wilayani Kyela mkoani Mbeya, wameendelea kuuza pombe zilizofungashwa katika mifuko ya plastiki vilivyopigwa marufuku na Serikali kwa kuvibatiza jina jipya la ‘chapati’ na ‘kichwa’.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA hivi karibuni, umebaini kuuzwa kwa viroba hivyo katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Kyela Stendi Kuu ya mabasi na maeneo mengine.

Viroba hivyo hutofautiana kutokana na mahali vinapotoka kwani vile vya Tanzania huitwa kichwa na vile vya kutoka nchini Malawi vikiitwa chapati.

Wakizungumzia hali hiyo jana bila kutaka majina yao yatajwe gazetini, baadhi ya wanywaji walisema hatua ya Serikali kudhibiti viroba wilayani Kyela huenda zikagonga mwamba kutokana na kuwa na soko kubwa kuliko pombe nyingine.

“Ndugu mwandishi naomba jina langu lihifadhi, grosery zote unazoziona hapa wanauza viroba kwa mwendo wa kificho, kama Serikali haitafanya operesheni ya kutosha mkakati huo utakwama,” alisema kijana mmoja katika eneo la Stendi kuu.

Katika maeneo mengine viroba huwekwa kwenye debe au ndoo kisha muuzaji hukaa juu yake na kuviuza kwa watu anaowafahamu pekee huku karatasi za viroba hivyo zikifichwa kwa kutunzwa sehemu maalumu ili visionekane hadharani.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kyela kati, ambaye naye ni mmoja wa wamiliki wa maduka maeneo hayo, Timoth Livanda, alisema viroba hivyo huuzwa kwa kificho kutokana na Serikali kutoa muda mfupi kuviondoa sokoni.

Alisema wauzaji wengi walinunua viroba hivyo vyenye nembo ya TBS huku wakilipia mapato na hatua ya Serikali kutoa muda mfupi kimewaathiri wafanyabiashara wengi.

Alisema ipo haja kwa Serikali kutoa muda maalumu ili kuokoa mitaji ya wafanyabiashara ambao tayari walikwishanunua mzigo mkubwa.

Akizungumzia hali hiyo kwa simu jana Mkuu wa Wilaya hiyo, Claudia Kitta, alisema hana taarifa za kuwapo viroba vilivyobadilishwa majina na kuuzwa kwa kificho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles