24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAZUIA MKUTANO WA MBUNGE CHADEMA

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi, Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara,  limepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) kwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara mkoani Mara.

Mbunge huyo alipanga kufanya mikutano hiyo kuanzia jana hadi Januari 11 mwaka huu.

Katika barua iliyoandikwa na Mrakibu wa Polisi aliyejitambulisha kwa jina la I. Kimasa kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tarime kwenda kwa Matiko, mbunge huyo ameagizwa aahirishe mikutano yake hadi Waziri Mkuu Majaliwa atakapokamilisha ziara yake.

“Kutokana na sababu za kiusalama kuhusiana na ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, unashauriwa kuahirisha mikutano yako ya hadhara kwenye viwanja vyote ulivyotoa taarifa. Mikutano hiyo ifanyike baada ya ziara ya waziri mkuu,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo, Matiko akizungumza na MTANZANIA, alipinga hatua hiyo kwa madai kuwa inakwenda kinyume na sheria na haki za mbunge.

Katika maelezo yake, Matiko alisema amejijengea utaratibu, kwamba kila akimaliza kuhudhuria vikao vya Bunge, hurudi jimboni kukutana na wananchi wake na vikundi mbalimbali na kuwapa mrejesho kutokana na yale waliyomtuma bungeni.

“Nikiwa jimboni nina wajibu wa kuzunguka kwenye kata zangu na kuwaeleza wananchi wangu ni yapi nimeyafanya bungeni na kuchukua kero zao niende nazo bungeni na zingine tuweze kuzitatua katika ngazi ya halmashauri.

“Niliandika barua kwenda kwenye ofisi ya OCD Wilaya ya Tarime kuwajulisha kwamba niko jimboni na nitakuwa nafanya ziara na niliainisha mikutano mitatu.

“Cha ajabu wameniletea barua na kusema kuwa niahirishe mikutano hadi ziara ya waziri mkuu ipite……

Kwa habari zaidi, jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles