24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

NEC YAWAONYA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

Na ASHA BANI–DAR ES SALAAM


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewaandikia barua za kuwatahadharisha wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kutojihusisha na siasa katika maeneo yao ambayo yanafanya uchaguzi wa marudio ya ubunge.

Kauli hiyo, ilitangazwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima, wakati wa kikao ilichoitisha cha viongozi wa vyama vya siasa, jeshi la polisi, Serikali na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Tumewaandikia barua viongozi wakiwamo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuwaeleza mipaka yao ya kazi ili wasiingiliane na siasa, wakati huu wa uchaguzi wa marudio katika majimbo yao.

“Tunaamini kufanya hivi kutasaidia kuwakumbusha kwa namna moja au nyingine kutimiza wajibu wao bila kuingilia masuala ya uchaguzi…ni imani yetu watazingatia kama barua zilivyoelekeza,”alisema Kailima.

Kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, alisema  matayarisho yamekamilika sambamba na wasimamizi wa uchaguzi 168 kupatiwa mafunzo .

Alisema uchaguzi wa marudi katika majimbo ya Songea Mjini, Singida Kaskazini na Longido utaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na endapo kutakuwa na malalamiko, ni vyema viongozi wa siasa wakatoa malalamiko sehemu husika.

“Uchaguzi huu utafanyika Januari 13, mwaka huu, naamini utakuwa huru na haki, napenda kuwatoa hofu wananchi na Watanzania wote kila kitu kitasimamiwa kwa mujibu wa sheria,”alisema.

Alisema pia uchaguzi kama huo, utafanyika katika majimbo ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni, Dar es Salaam, Febaruari 17, mwaka huu.

Alisema matatizo yote, ikiwamo malalamiko ya kuwaondoa mawakala jeshi la polisi yamepokelewa na yataanza kushuhulikiwa haraka.

WAPINZANI

Katika hatua nyingine, viongozi wa vyama vya upinzani, walilalamikia Jeshi la Polisi kwa kuwanyanyasa wakati wa uchaguzi na hasa chaguzi ndogo.

Katika mkutano huo, vyama Chadema na CUF,  havikutuma wawakilishi wao, licha ya kupewa mwaliko.

Itakumbukwa Chadema ilitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa  madai mbalimbali, yakiwamo ya kutotendewa haki na wafuasi wao kupigwa na polisi wakati wa uchaguzi mdogo wa kata 43.

Viongozi wengi, wamelalamikia hatua ya polisi kuwa sehemu ya chama tawala na kufanya kazi za kuwanyanyasa kinyume na haki za binadamu.

Akichangia hilo, Naibu Katibu Mkuu (Bara) wa Chama cha ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, alisema jeshi hilo linatumika vibaya kipindi cha uchaguzi  kwa kuwakamata wapinzani kila wakati.

“Jeshi la Polisi linatumika,ndiyo chanzo cha migogoro katika chaguzi mbalimbali, unafikiri kwa nini Chadema hawapo hapa si kwa sababu chaguzi haziendi kwa haki, lazima mkubali polisi mnatumika vibya.

“Acheni kuwatumia polisi kwanza, kwa nini wafike kwenye uchaguzi wakiwa wamevalia sare zao, hii inawatisha hata wapiga kura jambo hili lazima lishughulikiwe,’’alisema Mtemelwa.

Alisema mbali na Jeshi la Polisi pia kuna wakurugenzi ,wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nao wanatumika vibaya na ni makada wa CCM, hivyo katika kuhakikisha wanashinda wanajiingiza na kufanya siasa…….

Kwa habari zaidi, jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles