Polisi wamkamata tena Kizza Besigye

0
633
KIONGOZI wa upinzani Uganda, Dk. Kizza Besigye
KIONGOZI wa upinzani  Uganda, Dk. Kizza Besigye
KIONGOZI wa upinzani Uganda, Dk. Kizza Besigye

KAMPALA-UGANDA

KIONGOZI wa upinzani  Uganda, Dk. Kizza Besigye alikamatwa na polisi juzi alipokuwa akitoka nyumbani kwake Kasangati wilayani Wakiso.

Muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake, Dk. Besigye kama kawaida yake, alirushiana maneno na Mkuu wa  wa Kituo cha Polisi Kasangati, Robert Kachumu.

Dk. Besigye alikamatwa baada ya kutomjibu ofisa huyo wa polisi ambaye alitaka kujua alikokuwa anakwenda kiongozi huo wa upinzani ambaye aliwahi kujitangaza mshindi na kujiapisha kabla ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu uliopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here