24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi: Vyama vya siasa ruksa mikutano ya ndani

Kamishna wa Mafunzo na Oparesheni, Nsato Mssanzya.
Kamishna wa Mafunzo na Oparesheni, Nsato Mssanzya.

Na HERIETH FAUSTINE, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi limeondoa zuio la mikutano ya ndani ya vyama vya  siasa likisema limeridhishwa na hali ya usalama iliyopo sasa.

Awali, jeshi hilo lilipiga marufuku mikutano yote ya ndani ya vyama vya siasa kwa madai kuwa ilikuwa inachochea wananchi kutotii sheria za nchi na kupandikiza chuki dhidi ya serikali.

Akizungumza   Dar es Salaam jana, Kamishna wa Mafunzo na Oparesheni, Nsato Mssanzya, alisema kuruhusiwa kwa mikutano hiyo kumetokana na jeshi hilo kuridhishwa na hali ya usalama iliyopo nchini.

“Jeshi la Polisi limekuwa likifuatilia hali ya usalama hasa inayohusiana na shughuli za vyama vya siasa na baada ya kujiridhisha kuwapo hali hiyo tumeona hakuna haja ya kuendelea kuizuia mikutano ya ndani.

“Leo tunaondoa katazo la mikutano ya ndani ya vyama vya siasa,”alisema   Mssanzya.

Alisema kwa sababu mikutano hiyo ni kwa mujibu wa katiba, jeshi limeruhusu kuendelea kufanyika   ikizingatiwa masuala yanayojadiliwa ni ya  utendaji zaidi.

“Hata hivyo ikitokea ndani ya mikutano hiyo kukawapo na mtu au kikundi chochote kitakachochochea uvunjifu wa sheria, hatutasita kumchukulia hatua za sheria ikibidi kumshusha pale alipo,”alisema.

Mssanzya alisisitiza kuwa maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa itaendelea kuzuiwa isipokuwa ile ya wabunge katika majimbo yao.

“Zuio la maandamano na mikutano ya hadhara liko pale pale hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika,”alisema.

Alisema jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi na vyama vya siasa kuheshimu sheria za nchi wakati wote na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles