33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hillary Clinton aongoza kura za maoni

Hillary Clinton
Hillary Clinton

WASHINGTON, Marekani

KURA za maoni za taifa za urais  Marekani zimekuja na habari njema kwa kambi ya mgombea urais wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton.

Hiyo ni baada ya kuonyesha akiongoza kwa tofauti ya asilimia sita dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump.

Clinton aliungwa mkono na asilimia 43 ya wapiga kura waliohojiwa katika utafiti huo ulioendeshwa kwa pamoja na mashirika ya habari ya NBC na The Wall Street Journal, kulinganisha na Trump aliyepata asilimia 37 ya kura.

Mgombea urais wa chama cha Libertarian, Gary Johnson aliendelea kushikilia nafasi ya tatu baada ya kupata asilimia tisa ya kura huku wa chama cha Green, Jill Stein akiambulia asilimia tatu ya kura hizo.

Awali, baada ya Mkutano Mkuu wa Democratic Julai mwaka huu, kura za maoni zilikuwa zikionyesha Clinton anaongoza kwa asilimia 10 kabla ya wiki za karibuni wagombea hao kuonekana wakikaribiana, kufungana au Trump kuongoza kwa asilimia chache.

Utafiti uliofanywa na mashirika ya habari ya Fox News na CBS/New York Times wiki iliyopita ulionyesha kukaribiana kwa wagombea hao.

Lakini leo hii, Clinton amerudisha uongozi wake kwa kiasi kikubwa tangu Agosti 31, wakati kura za maoni zilizoendeshwa na Fox News zilipoonyesha akiongoza kwa asilimia sita.

Clinton aliungwa mkono zaidi na wapiga kura wa kiume kwa mujibu wa kura za maoni zilizoendeshwa na NBC/Wall Street Journal.

Trump aliendelea kuungwa mkono kwa kiwango kikubwa na makundi ya  jamii, akiwa na asilimia 46 ya kura dhidi ya Clinton aliyepata asilimia 44, ikiwa ni asilimia ndogo mno tofauti na utafiti wa hivi karibuni.

Hali kadhalika, waliohojiwa walieleza wasiwasi kuhusu maneno na matendo ya Trump katika kampeni huku asilimia 69 wakiripoti kuwa na shaka na kampeni yake na asilimia 54 wakisema wana ‘wasiwasi mkubwa.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles