31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Naibu Meya aburuzwa kizimbani

Prosper Msofe
Prosper Msofe

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA

ALIYEKUWA Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Prosper Msofe (Chadema), amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujipatia Sh milioni nane kwa udanganyifu.

Prosper ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akidaiwa kutafuna fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa maji.

Pamoja na Msofe, mwingine aliyepandishwa mahakamani hapo kwa shtaka hilo ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Daraja Mbili, Modestusi Lupogo.

Watuhumiwa wote wawili walisomewa mashitaka yao katika kesi namna 379 mbele ya Hakimu Augustine Rwezile.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Monica Kijazi akisaidiana na Wakili Mwandamizi, Rehema Mteta, alidai watuhumiwa wanakabiliwa na makosa matatu wanayodaiwa kuyafanya kati ya Oktoba mosi na Novemba 2013.

Wakili Kijazi alidai mtuhumiwa Lupogo anakabiliwa na shitaka la  kwanza ambalo ni kudaiwa kufanya udanganyifu katika nyaraka kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kupambana na Rushwa.

Alidai mtuhumiwa akiwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Daraja Mbili, aliwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka 2013 akionyesha Sh milioni nane zilitumika katika mradi wa maji katika Mtaa wa Alinyanya na Sanare.

Shtaka la pili liliwakabili watuhumiwa wote wawili ambalo ilidaiwa katika kipindi hicho, walishirikiana kutenda ubadhidhilifu wa fedha za umma kinyume na kifungu cha 32 cha sheria za Takukuru.

Wakili Kijazi akisoma shitaka la tatu lililowahusu watuhumiwa wote wawili alidai kwa nafasi walizokuwa nazo, watuhumiwa hao walikwenda kinyume na kifungu cha 28 (i) cha sheria za kupambana na rushwa ambako walijipatia kiasi hicho cha fedha, mali ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Washtakiwa walikana mashtaka na kudhaminiwa hadi Oktoba 11 mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles