29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

Polisi Uganda yatoa picha za CCTV dhidi ya tukio la Jenerali Wamala

Kampala, Uganda

Jeshi la Polisi Nchini Uganda wametoa picha za mtaani za CCTV za watuhumiwa wawili wanaoaminiwa kuhusika na shambulio la kumuua Jenerali na Waziri wa uchukuzi nchini humo, Katumba Wamala.

Gari la Jenerali Katumba Wamala lilipigwa risasi na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki, na kumuua binti yake pamoja na dereva.

Picha za video za CCTV zinawaonesha watu wawili huku mmoja wao amevalia fulana ya blue yenye mistari na hakuna hata sura ya mmoja wao inayoweza kutambulika.

Pia moja ya pikipiki hizo iligeuza eneo ambalo sio mbali kutoka eneo la tukio la shambulio, kabla ya kutoweka ndani ya kituo cha petroli.

Kikosi cha pamoja cha ujasusi cha polisi, na jeshi kinachunguza tukio hilo la Waziri na Jenerali, Wamala kufyatuliwa  risasi.

Jeshi linasema linachunguza simu ambazo zinaonekana kuwa zilitumiwa kufanya mpango wa jaribio la mauaji.

Hata hivyo nchi ya Uganda imerekodi mashambulio kadhaa ya aina hiyo ya watu maarufu katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,310FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles