23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Polepole amkabidhi Shaka mikoba ya Uenezi CCM

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Katibu Mkuu wake, Daniel Chongolo kwa kuanza kutoa Mwelekeo na dira ya majukumu ya Sekretariet ya NEC kwa muktadha wa kuisimamia na kufuatilia utendaji wa Serikali utakoleta tija na manufaa kwa umma.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Chama hicho kimesema Sekreteriet ya NEC haitakuwa tayari kuona Watanzania wakihangaika, kutaabika na kukosa haki za msingi au wakifanyiwa dharau na udhalilishaa wa aina yoyote.

Msimamo huo umeelezwa jana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza hayo wakati wa makabidhiano kati yake na aliyekuwa Katibu wa Idara hiyo, Humphrey Polepole, Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Shaka alisema ni kawaida yanapotokea mabadiliko wahusika kukabidhiana kazi za kiofisi na kuongeza kusema kama kazi ya utendaji  za CCM, Katibu Mkuu Chongolo ni kama upele ulimopata mkunaji kutoka na upeo alionao kisiasa na kiutendaji.

Shaka alisema atakuwa tayari kutumia kila alichonacho kusaidiana na wenzake lakini pia yuko tayari kupokea na kujifunza kutoka kwa wenzake akichukua na kupokea mawazo, ushauri, miongozo na kuwa umjasiri wa kusimamia changaomoto chini ya shabaha na malengo ya CCM. 

Alizitaka taasisi za umma na za kiserikali kla moja kutimiza wajibu wake kwa kutumikia na kufuata miongozo ya kisera na malengo ya kimkakati ilioainishwa kwenye ilanj ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25.

“Wote ni mashahidi Rais Samia Suluhu Hassan amechukua jitihada za wazi za kujenga mahusiano yanayochochea msukumo wa biashara na uwekezaji. Ameondoa vizuizi vya kibiashara kwa manufaa ya wote. Amewahimiza wafanyabiashara na wananchi kulipa kodi .Kodi isiwe bughudha na kuzuizi bali kila mmoja alipe kwa wakati na hiari,” alisema Shaka.

Alisema Rais Samia ana nia ya dhati na kweli amedhamiria kujenga nchi huku akitaka iende kwa mwendo wa haraka ndio maana ameanza kufungua milango iliotaka kujifunga akifuata nyayo za watangulizi wake ambao wote walipikwa, kuandaliwa na kupewa dhamana ya uongozi na CCM.

“Kwa dhamana nilionayo naahidi kuwa kiungo na daraja kwa watendaji wenzangu na makundi ya wanahabari, wanamichezo, wasanii na walemavu, Rais samia ameshasema upepo uwe mwingi au kidogo jahazi litatia nanga katika bandari ya mafanikio, CCM pia inaunga mkono msimamo huo na kutekeleza kwa vitendo,” alisisitiza.

Aidha Shaka aliawasihi viongozi wa taasisi za serikali, mamlaka, wakala mbalimbali za serikali na kujitafakari ili kuona muhimu wa kumuunga mkono Rais Samia kwa utendaji wenye tija hatimaye wananchi wanufaike na kufikia kilele cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Aidha, Shaka amemshukuru aliyekuwa Katibu wa Idara hiyo,Hamphrey Pole Pole kwa kazi aliyoifanya yeye na wenzake wote huku akiahidi kuacha wazi milango ya idara hiyo kwa namna yoyote ile ya kupokea ushauri kwa maslahi ya CCM kwa maendeleo ya Taifa. 

“Katibu Mkuu wetu amekusudia kuwa na chama linachotegemewa na wananchi nyakati  zote. CCM hakijawahi kuwa chama cha masetla hivyo kitaendelea kubaki ni chama cha wakulima na wafanyakazi chenye nia ya kujenga jamii ilio sawa na huru,” alisema Shaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles