30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TEF yapata safu mpya ya Uongozi

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wamepiga kura ya kuchagua wajumbe saba wa Kamati ya Utendaji ya jukwaa hilo, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.

Wajumbe hao wataungana na washindi wa nafasi ya Mwenyekiti, Deodatus Balile na Makamu Mwenyekiti, Bakari Machumu walioshinda katika uchaguzi huo na kutangazwa na Kamati ya Uchaguzi ili kuliendesha jukwaa hilo katika kipindi cha miaka minne.

Walioketi ni kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Makamu Mwenyekiti Bakari Machumu. Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliosimama kutoka kushoto ni Lilian Timbuka, Simon Mkina, Yassin Sadick, Jane Mihanji, Salim Said Salim, Angela Akilimali na Neville Meena.

Walioshinda ni Salim Said Salim, Yassin Sadick, Simon Mkina, Neville Meena, Jane Mihanji na Lilian Timbuka.

Wagombea katika bodi hiyo walikuwa 11 ambao ni Nevile Meena (62 ), Taus Caren Mbowe (45), Jane Mihanji (63), Lilian Timbuka ( 55), Sadik Yassin (69).

Wengine ni Angel Akilimali ( 48), Simon Mkina (69),Salim Salim Kura (75), hata hivyo wagombea, Saed Kubenea na Joyce Shebe walijitoa katika kinyang’anyiro hicho. Hivyo wagombea saba ndio walipitishwa kuwa wajumbe wa bodi ya TEF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles