23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Jezi mpya za Meridian Bet zaipa mzuka LCL kwenye ligi Kuu ya Walemavu

Msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet umeipa mzuka timu ya Lenster senior league (LCL) wa kushinda ubingwa tena wa Ligi Kuu ya walemavu itakayoanza Juni mwaka huu.

Timu hiyo yenye wachezaji saba wa timu ya taifa imekabidhiwa msaada wa jezi, vikinga ugoko, njumu, mipira na soksi vilivyotolewa na Meridian Bet.

Meneja wa Meridian Bet, Ernest John na Meneja Mwendashaji Mkuu Tanzania, Corrie Borman walikabidhi msaada huo katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Meridian Bet na kueleza kuwa ni muendelezo wa kampuni yao kusaidia jamii yenye uhitaji nchini.

Nahodha wa LCL, Alphan Athuman aliyeambatana na wachezaji wengine na uongozi wa timu amesema msaada huo ni chachu kwao kufanya vizuri na kuuahidi uongozi wa Meridian Bet kurejea na kombe mwishoni mwa msimu baadae mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles