28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Pochettino aacha ujumbe mzito Tottenham

LONDON, ENGLAND 

BAADA ya kocha Mauricio Pochettino kufungashiwa virago na Tottenham mapema wiki hii, kocha huyo ameacha ujumbe mzito kwa wachezaji ambao unaonekana kuwagusa kila mmoja wao.

Kocha huyo raia wa nchini Argentina amefukuzwa kazi Jumanne wiki hii na nafasi yake ikichukuliwa na Jose Mourinho saa chache baada ya kufukuzwa kwake.

Pochettino amekuwa ndani ya kikosi hicho tangu mwaka 2014, huku msimu uliopita alifanikiwa kuipeleka timu hiyo hadi fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati Pochettino anafukuzwa kazi idadi kubwa ya wachezaji walikuwa wapo katika timu zao za taifa, hivyo hakuweza kuwaaga, lakini kocha huyo aliamua kutumia nafasi yake kuacha ujumbe mzito kwenye ubao wa kufundishia kwa ajili ya wachezaji waone mara baada ya kurudi kwenye kiwanja chao cha mazoezi Enfield Training Centre.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Pochettino, Jesus Perez, alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuposti picha ya kocha mkuu akiwa anaandika ujumbe huo.

“Asante sana kwenu wachezaji wote, tumekosa muda wa kuwaaga, lakini kaeni mkijua kwamba mtaendelea kuwa kwenye mioyo yetu,” aliandika kocha huyo.

Ujumbe huo umewaacha midomo wazi baadhi ya wachezaji ambao wanaamini walikuwa wanapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wake na wengine hawana imani ya namba kwenye kikosi chini ya Mourinho.

Pochettino amekuwa akihusishwa kutaka kukimbilia nchini Ujerumani katika mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini humo, Bayern Munich, ambayo kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Hansi Flick kwa muda baada ya kocha mkuu Niko Kovac kufukuzwa.

Kwa upande mwingine kocha huyo amekuwa akihusishwa kuwindwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania, Barcelona kwenda kuchukua nafasi ya Ernesto Valverde ambaye yupo hatarini kufungashiwa virago.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles