22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Man City, Chelsea hapatoshi England leo

MANCHESTER, ENGLAND

KIVUMBI cha michuano ya Ligi Kuu nchini England, kinatarajia kuendelea leo kwenye viwanja mbalimbali huku mchezo ambao unatarajiwa kuteka hisia za wengi ni kati ya mabingwa watetezi Manchester City dhidi ya Chelsea inayofanya vizuri chini ya kocha Frank Lampard.

Manchester City kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo 12, huku Chelsea wakiwa wanashika nafasi ya tatu, nafasi ya pili ikishikwa na Leicester City na Liverpool wakiwa wanaongoza kwenye msimamo huo.

Chelsea imekuwa na ushindani wa hali ya juu msimu huu tangu ikiwa chini ya Lampard baada ya Maurizio Sarri kuondoka na kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus, lakini kwa upande wa Manchester City chini ya kocha wao Pep Guardiola timu hiyo imeanza vibaya, hivyo leo kutakuwa na ushindani wa hali ya juu huku kila timu ikitafuta matokeo ya kujiweka sawa kwenye msimamo wa Ligi.

Katika michezo minne ambayo Chelsea wamecheza ugenini dhidi ya Manchester City, wameshinda mmoja na kufungwa mitatu, hivyo na leo watakuwa ugenini kwenye uwanja wa Etihad.

Katika historia ya timu hizo zimekutana jumla mara 148, lakini Chelsea wameonekana kuwa wababe kwa Manchester City, huku Chelsea ikiwa imeshinda mara 58, wakati huo Manchester City ikishinda mara 51 na wakitoka sare mara 39.

Hivyo mchezo wa leo utakuwa na ushindani wa hali ya juu kwa kuwa Guardiola anataka kurudisha heshima yake, wakati huo Lampard akitaka kuonesha ubora wake.

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Tottenham ambayo ipo chini ya kocha Jose Mourinho wakiwa ugenini dhidi ya West Ham, wakati huo Bournemouth wakiwa nyumbani kucheza dhidi ya Wolves, Arsenal wao watakuwa nyumbani kupambana na Southampton.

Brighton watakuwa nyumbani kuwakaribisha Leicester City, wakati huo Liverpool wakifunga safari na kuwafuata Crystal Palace, huku Everton wakicheza dhidi ya Norwich City na Watford wakiwa nyumbani kupambana na Burnley.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles