25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

PILAU LILILOCHANGANYWA NA KUKU WA KIENYEJI

Mahitaji
 
Mchele    kilo 1
 
Kuku    1
 
Vitunguu 3
 
Viazi mbatata 5
 
Jira/binzari ya pilau vijiko vya supu 3 
 
Mdalasini    1 
 
Pilipili manga    kijiko cha supu 1 
 
Hiliki    chembe 3 
 
Karafuu    chembe 5 
 
Kitunguu saumu (thomu/galic) kilichoosagwa     vijiko vya supu    3 
 
Tangawizi mbichi iliyosagwa    vijiko vya supu 3 
Mafuta ya kupikia kikombe ½ 
 
Chumvi kiasi
 
 
Namna ya kupika
 
1.    Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu saumu na tangawizi
 
 
2.    Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
 
 
3.    Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
 
 
4.    Tia binzari zote isipokuwa hiliki.
 
 
5.    Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu saumu ukaange kidogo. 
 
 
6.    Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
 
 
7.    Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
8.    Ukiiva ipua, tayari kwa kuliwa. Chakula hiki unaweza kula kwa kachumbali na ndizi za kuiva pembeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles