22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Pemba wapewa elimu ya ardhi

Khamis Sharif – Pemba

WANANCHI kisiwani Pemba, wametakiwa kuvitumia ipaswavyo vyombo vya sheria wakati wa kumilikishana mali zao ili kupunguza kesi ambazo hujitokeza miongoni mwao.

Akizumza na masheha wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa nyakati tofauti kisiwani huko, wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar, Ali Hassan, alisema kesi nyingi za madai ya ardhi na kudhulumiana zinajitokeza na baadhi kushindwa kuendelea kwa sababu ya kukosekana ushahidi wa kutosha.

Alisema siku zote ardhi ni mali ya Serikali, hivyo mashamba hayafai kurithiwa wala kuuzwa bali watoto wanaweza kuyaomba wakamilikishwa kwa hati maalumu kwa matumizi ya kilimo na shughuli nyengine za maendeleo.

 β€œNa katika uuzaji wa ardhi ya mashamba yasiyokua ya eka lazima muuzaji apitie katika bodi ya uhaulishaji ardhi na hakikisheni anayemuuzia ni mzanzibari kama inavyosema sheria ya ardhi.

“Vile vile haki ya matumizi ya ardhi kutoka kwa mnunuaji na muuzaji haikamiliki hadi pale itakaposajiliwa kupitia kwa mrajisi wa mahakama ya ardhi,” alisema wakili huyo.

Aidha alisisitiza jamii kuwa wanaponunua viwanja au mashamba waandikishane.

 Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Zanzibar, Mtumwa Said Sandal, akizungumzia suala la udhalilishaji, alisema baadhi ya wanaume hawatekelezi majukumu yao katika familia na badala yake kuwaachia wanawake watekeleze, jambo ambalo ni udhalilishaji.

Alieleza kuwa  mtoto anapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kulelewa katika malezi ya kikatili anakua na makuzi mabaya na kusababisha  kuathirika kisaikolojia.

“Sheria ambazo zinasimamia vitendo hivo ni sheria ya makosa ya jinai namba 6 ya mwaka 2016, sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2017 na sheria ya mtoto namba  7 ya mwaka 2011,” alisema.

Naye, Mwanasheria wa Serikali kutoka ofisi hiyo,  Ali Issa Hassan, alisema ofisi yao ina jukumu la kuishauri Serikali katika masuala ya kisheria na kuitetea kwani pia inashitakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles