25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Papai ni dili kwa wavutaji wa sigara

papai

Na HERIETH FAUSTINE,

WATU wengi hupendelea kula tunda la papai kutokana na utamu wake, mbali na kuwa na utamu tunda hilo limekuwa na faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Asili ya mti wa mpapai ni kutoka Amerika ya kati ambapo umekuwa ukitumika kusaidia mwili wa binadamu kuanzia matunda, majani na utomvi wa tunda hili huweza kutumiwa kama dawa.

Licha ya kuwa tunda maarufu duniani na linalopendwa na watu wengi, papai pia limekuwa na faida nyingi na za pekee ambazo hupatikana hadi katika mbegu zake.

Faida kubwa ya tunda hili ni kusaidia katika mfumo  wa umenge’nyaji wa chakula (papain) ambavyo husaidia usagaji na ulainishaji wa chakula tumboni. Wakati mwingine vimenge’nyo hivyo hutumika kama dawa katika kutibu majeraha kwenye tumbo.

Pia papai husaidia kuzuia magonjwa ya moyo na kisukari kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin C, E na A ambazo zina nguvu katika kutoa kinga dhidi ya magonjwa hayo.

Vilevile mbegu za tunda la papai zinaliwa ingawa huwa na ladha ya uchungu lakini hazina madhara bali ni tiba. Pia zikikaushwa na kusagwa kuwa unga hutibu malaria, ini, homa huku majani yake husaidia kutibu shinikizo la damu.

Hali kadhalika mizizi ya mmea wa mpapai husaidia kuzuia kutapika, lakini pia papai linaweza kutumika kama kilainisho cha nyama ili iweze kuiva vizuri, hususani nyama ya ng’ombe.

Papai ndiyo chanzo kikuu cha virutubisho ambavyo hutoa kinga kubwa ya mwili (antioxidant) kama vile Carotenes, vitamin C, Flavonoids na jamii zote za vitamin B, mbali na hayo lina madini ya Potassium, Magnesium na Fiber.

Tunda la papai pia huboresha afya ya mapafu kwa wavutaji wa sigara au kwa watu ambao wapo katika mazingira yenye moshi wa sigara, kama vile katika kumbi za starehe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles