PAPA FRANCIS AKOSOA UJENZI WA KUTA KUZUIA WAHAMIAJI

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amesema viongozi wa kisiasa wanaotaka kujenga kuta na kuweka vizuizi vingine kuwazuia wahamiaji watabaki kuwa wafungwa wa kuta hizo.

Papa Francis ametoa matamshi hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu uhamiaji na kitisho cha rais Donald Trump wa Marekani cha kufunga mpaka wa kusini na Mexico.

Ingawa hakumtaja rais Trump kwenye majibu yake, ametofautiana naye kuhusu suala la uhamiaji ambalo lilirudiwa mara kwa mara kwenye maswali mengi aliyoulizwa wakati yeye na ujumbe wake walipokuwa wakielekea na kurudi kutoka ziarani Morocco.

Akilizungumzia tatizo hilo jana mbele ya viongozi wa Morocco, alisema halitaweza kushughulikiwa kwa vizuizi, na badala yake kunahitajika haki ya kijamii na kurekebisha hali ya kukosekana kwa usawa wa kiuchumi duniani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here