25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Wanaume wanaowatumikisha anawake wajawazito waonywa

SHOMARI BINDA

MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amesema itafikia hatua wanaume watakaowatumikisha wake zao wajawazito kazi ngumu wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hiyo ni katika  kupambana na vifo vinavyotokana uzazi vinavyotokea kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitalini.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizindua kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vinavyotokana na uzazi yenye kaulimbiu “Maneno basi sasa vitendo” kupitia mradi wa Jiongeze Tuwavushe Salama uliozinduliwa mkoani Mara.

Alisema yapo mambo mengi yanayochangia kutokea vifo vinavyotokana na uzazi na ipo mipango na mambo ambavyo yanaweza kufanywa kuhakikisha vifo hivyo vinapungua na kumalizika iwapo kutakuwa na ushirikiano kuanzia kwa viongozi na jamii kwa ujumla.

Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa afya kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara.

Malima alisema wapo wanaume ambao licha ya mama kuwa na ujauzito wa kukaribia kujifungua   bado anatumikishwa kazi ngumu zinazohatarisha maisha yake.

Alisema katika maeneo mengi hususan ya vijijini wapo wanawake wajawazito ambao waume zao wanawalazimisha kwenda kuchunga ng’ombe kwa saa nyingi na hata kulimashambani huku wao wakikaa vijiweni jambo ambalo haliwezi kukubalika.

“Tunaposema tuwavushe salama yapo mambo mengi ya kuzingatia juu ya mama wajawazito katika kuwaepusha na vifo vinavyotokna  na uzazi kwa kuwa wapo wanaume ambao wanachangia kwa asilimia kubwa kutokea kwa vifo hivi.

“Sasa tutakapokuwa kwenye maeneo yetu kama viongozi na tukamuona mama mjamzito anachunga ng’ombe au kufanya kazi ngumu ambazo tutaona hazistahili kwa hali yake tumtafute mume wake au aliyempa ujauzito ili akamatwe,”alisema Malima.

Meneja wa Shirika la Jhipiego “Boresha Afya” Mkoa wa Mara, Mwakajonga Tuntufye, alisema kila mmoja anapaswa kuchukua hatua katika kampeni hiyo kwenye eneo lake na isichukuliwe suala hilo linapaswa kufanywa na mtu fulani.

Alisema yapo mambo mambo mengi ambayo yanasababisha  vifo vinavyotokana na uzazi ikiwa ni pamoja na mama wajawazito kushindwa kufika mapema kliniki.

Alisema kwa sababu hiyo  ni muhimu kukumbushwa kufika mapema mara baada ya kupata ujauzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles