21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

UN: BADO INAWEZEKANA KUDHIBITI MABADILIKO YA TABIANCHI

Ulinzi wa sayari dunia unahitajika haraka hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Katika ujumbe wake maalumu kwa ajili ya “saa ya sayari dunia” hii leo Guterres amesema “tunashuhudia athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi , kupotea kwa bayoanuai, uchafuzi wa bahari, mmomonyoko wa udongo na uhaba wa maji .”

Hata hivyo amesema habari njema ni kwamba kuna suluhisho, Bado inawezekana kudhibiti mabadiliko ya tabianchi , kulinda sayari yetu na kuhifadhi mustakabali wetu kwani teknolojia iko upande wetu”.

Ameongeza kuwa anaitisha mkutano wa kimataifa wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mwezi Septemba mwaka huu na anawataka viongozi wa dunia kuja na mipango madhubuti.

Amesisitiza kwamba saa ya sayari dunia ni fursa ya kuonyesha mshikamano na hatua bora dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuzima taa Jumamosi hii ya Machi 30 kuanzia saa mbili na nusu usiku saa za New York. 

Guterres ametoa wito “Kwa pamoja hebu tujenge mustakabali bora, safi, salama na unaojali mazingira kwa ajili ya kila mtu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles