21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Papa alaani mashambulizi barani Afrika

VATICAN CITY

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ametumia hotuba yake ya Krismasi kukemea matukio ya kigaidi na siasa kali Magharibi mwa Afrika, ikiwa ni siku moja baada ya wanamgambo kuwauwa watu 35 nchini Burkina Faso.

Akitoa ujumbe wake mjini Vatican hivi jana, Papa Francis alilaani mashambulizi dhidi ya Wakristo barani Afrika na kuwaombea wahanga wa mizozo, majanga ya kimaumbile na maradhi kwenye bara hilo.

Papa pia alitoa wito wa kufarijiwa wale wanaoadhibiwa kwa ajili ya imani zao za kidini, hasa wamishionari na waumini waliotekwa na wahanga wa mashambulizi ya makundi ya itikadi kali, hasa nchini Burkina Faso, Mali, Niger na Nigeria.

Kauli ya Papa Francis imekuja wakati kukiwa na ripoti kwamba wanamgambo wa itikadi kali nchini Burkina Faso wamewauwa watu 35, wengi wao wanawake, baada ya kushambulia maeneo mawili tofauti kwa wakati mmoja kwenye mji mmoja wa kaskazini mwa nchi hiyo na kambi ya kijeshi.

Katika hotuba yake ya Krismasi, mbali na kutaja matukio ya kigaidi barani Afrika, Papa Francis aliwaombea pia wale wanaoteseka kutokana na ghasia, majanga ya kimaumbile au mripuko wa maradhi, na pia wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari kuingia barani Ulaya kusaka maisha bora.

“Ni dhuluma ndiyo inayowafanya wavuke majangwa na bahari ambazo huwa makaburi yao,” alisema kwenye ujumbe wake wa “Urbi et Orbi” (Kwa Mji na kwa Ulimwengu) katika makao makuu ya kanisa hilo, Vatican.

Mashambulizi ya juzi jumanne nchini Burkina Faso yanatajwa kuwa mashambulizi mabaya kabisa kuwahi kufanywa katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika, ambalo limekuwa likishuhudia mashambulizi ya makundi ya kigaidi kwa kipindi kirefu sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,590FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles