23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mzee aiba pesa na kuzitoa kama zawadi

COLORADO, MAREKANI

Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe alifanya uvamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.

Polisi wamethibitisha “mwanaume mzee wa kizungu” alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.

“Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu,” shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado’s 11 News.

“Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, ‘Merry Christmas!'”

Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mgahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.

Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.

Polisi wamemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye miaka 65. 

Polisi hawajabaini kuwa huenda alikuwa na usaidizi wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles