26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

‘PANYA ROAD’ WATEKETEZA MAGARI 80 SWEDEN

STOCKHOLM, SWEDEN


KUNDI la kiuni la vijana, linadaiwa kuchoma na kuyatetekeza kwa moto magari zaidi ya 80 nchini hapa.

Habari kutoka mjini hapa zinaeleza tukio hilo lilitokea juzi usiku katika mji wa Gothenburg uliopo magharibi mwa nchi na linaonekana lilipangwa.

Waziri Mkuu, Stefan Lofven, alisema tukio hilo linaonekana kama ni la oparesheni iliyopangwa kijeshi kutokana na jinsi lilivyoendeshwa.

Alisema mbali na mji huo, pia matukio ya uchomaji magari yaliripotiwa katika mji wa Falkenberg ambao upo kusini mwa nchi.

Vyombo vya habari vya hapa vinaeleza matukio hayo yamekuwa yakiendeshwa na kundi la vijana wadogo ambao wamekuwa wakivunja vioo vya magari, huku wakiwarushia mawe maofisa wa polisi.

Maofisa wa polisi wanasema walishawatambua baadhi ya vijana hao na wamewataarifu wazazi, lakini hawakuweza kuwataja.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,740FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles