24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

MWALIMU ALIYEMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI JELA MIAKA MITANO

BUJUMBULA, BURUNDI


MAHAKAMA ya Burundi imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela mwalimu mkuu ambaye alikamatwa hivi karibuni akimfanyia mtihani wa taifa mwanafunzi.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mbali na kifungo hicho, mahakama hiyo pia imemfungia mwalimu huyo, Benjamin Manirambona kutojihusisha na shuhghuli yoyote ya kufundisha ama kuajiriwa katika ofisi ya umma kwa kipindi cha miaka 10.

Mwalimu huyo alikamatwa Ijumaa wiki iliyopita na polisi aliyekuwa aliyeingia katika chumba cha kufanyia mtihani akiwa amevaa sare za wanafunzi.

Baada ya kukamatwa, mwalimu huyo wa Chuo cha Ufundi cha Butere kilichopo mjini hapa, alikiri makosa na akasema alikuwa akimfanyia mtihani ofisa mmoja wa jeshi ambaye anafanya kazi ya kulinda amani nchini Somalia.

Katika maelezo hayo, mtuhumiwa huyo alisema ofisa huyo alikuwa akihitaji ufaulu wa juu ili aweze kujiunga na Chuo Kikuu.

Alisema mwanajeshi huyo alimuahidi malipo wakati atakaporejea akitokea Somalia.

Hata hivyo, Waziri wa Elimu, Janvière Ndirahisha, ambaye aliwasili eneo la tukio akiwa na askari waliokuwa wamevaa sare, aliyakataa maelezo ya   Manirambona akisema ni ya uongo.

“Kila kitu ambacho unakizungumza ni cha uongo, kwahiyo tunakuchukua na tutakuchunguza kwa jinsi tulivyosikia sio mara ya kwanza kufanya hivyo,” alieleza waziri huyo.

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni mhasibu wa chuo hicho, Eric Nkurunziza na mwalimu Lazard Nihezagire, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili na kufungiwa kufanya kazi katika ofisi za umma kwa muda wa miaka mitano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles