Owan Golden aachia video ya ‘Addicted’

0
311

New Brunswick, Canada

Baada ya kufanya vizuri na audio ya wimbo, Addicted, msanii wa kizazi kipya nchini Canada, Owan Golden, muda wowote kutoka sasa anatarajia kuachia video ya ngoma hiyo.

Owan anayewakilisha vyema Afrika Mashariki, ameiambia www.mtanzania.co.tz kuwa video hiyo iliyofanyika Canada itaongeza ukubwa was wimbo huo kutokana na uzuri wake.

“Nashukuru kwa mapokezi mazuri ya audio ya Addicted, Jumatatu hii naachia video yake hivyo naomba sapoti kwa mashabiki zangu kama vile ambavyo mmekuwa mkinipa siku zote ili East Africa izidi kuwa kwenye ramani, unaweza kufuatilia kazi yangu kupitia Instagram @owan_official na video itakuwa kwenye chaneli yangu ya YouTube,” amesema Owan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here