Erica Lulakwa atoa siri ya ‘Chereko’

0
329

California, Marekani

Msanii wa kikazi kipya anayeishi nchini Marekani, Erica Lulakwa a.k.a Twiga, amesema anashukuru kwa mapokezi makubwa ya wimbo wake, Chereko aliouachia hivi karibuni.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Erica amesema ngoma hiyo ina maajabu kutokana na uzuri wake kila mtu atakayesikiliza anavutiwa huku akijivunia kuendelea kutumia lugha ya Kiswahili licha ya kuwa anaishi Marekani.

“Naendelea kutumia Kiswahili katika nyimbo zangu sababu ndo lugha mama pili napenda muziki wangu ueleweke kwa Watanzania pia hii ni njia moja wapo ya kuitangaza lugha ya Kiswahili.

“Mpaka sasa Chereko imepokelewa vizuri sana na mtu yeyote akisikia anaipenda ghafla, inapatika majukwaa yote ya kidijitali ya kuuza na kusikiliza muziki pia video ya Chereko itatoka nipo naiandaa, nilitaka kuja fanyia video Tanzania ila nikisubiri mpaka kuja huko itachukua muda mrefu kwa hiyo naifanyia hapa Marekani,” amesema Erica.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here