22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Washiriki Miss Mwanza wakabidhi zawadi kituo cha Hisani Center

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

Washirika wa Shindano la Miss Mwanza 202 na Uongozi wao wametembelea kituo cha kulele watoto wenyewe uhitaji maalum Hisani Center wilayani Ilemela Buswera na kushiriki nao michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi walizoenda nazo Mkurugenzi wa shindano hilo, Sebastian Kaluguru, amesema moja ya kazi ya warembo ni kuwa karibu na jamii na kutoa huduma husika kwa wale wanaohitaji.

“Leo tumekuja kutembelea watoto ambao wanaishi katika kituo hichi cha Hisani Center, pamoja na zawadi ambazo zitawasidi katika maisha yao ya hapa nyumbani hii itakuwa ni endelevu tutatembelea vituo mbalimbali wakati hii wa kambi na baada ya kumaliza mashindano mshindi atakaye patikana ataendeleza mfumo huu,” anasema Kaluguru.

Aliongeza kuwa jamii haipaswi kuwasahau watoto wanaoishi katika mazingira magum hivyo ameomba mashirika, taasisi na serekali kuwa kumbuka mara kwa mara na kuunda kampeni pamoja na sera zitakazo wasaidi kujikwamua.

Kwa upande wa mlezi wa kituo hicho, Grece Pita ameshukuru uongozi wa miss Mwanza na kuwakaribisha watu ambao wana uwezo wa kuwasaidi watoto hao kwa upande wa chakula, elimu na afya na ushauri kujitokeza.

“Nichukuwe nafasi hii kuiomba jamii kutembelea vituo hivi vya kulelea watoto kujua mahitaji yao, kuwashauri pamoja na kutenga muda wa kucheza nao ni faraja kubwa wanavyo ipata,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles