Esther Makuba awabariki mashabiki na ‘Because of You’

0
360

Mwanamuziki mahiri wa Injili kutoka nchini Marekani, Esther Makuba, amegusa mioyo ya wapenzi wa muziki huo kupitia video ya wimbo wake mpya, Because of You.

Akizungumza na mtanzania.co.tz , Esther, amesema anawashukuru mashabiki kwa uvumilivu wao mpaka video hiyo imetoka na imewabariki watu wengi.

“Baada ya muda mrefu sasa nimetoa video ya Because of You, ni wimbo wa kuabudu ambao natamani umhudumie kila mmoja wetu, video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube ya Esther Makuba,” amesema mwimbaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here