28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

OPERESHENI ONDOA MIFUGO YAJA NGORONGORO

 

 

Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA

WILAYA ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), litaendesha operesheni ya kuondoa idadi ya wafugaji waliovamia maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Pamoja na operesheni hiyo, watakaohamishwa watafikishwa mahakamani kwa kosa la kulisha mifugo katika maeneo ya hifadhi kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mkuu wa Wilaya ya Ngongoro, Rashid Mtaka, alisema operesheni hiyo itafanyika wakati wowote baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mtaka alisema yeye kama kiongozi wa Serikali, anawajibika kulinda rasilimali za umma ikiwamo hifadhi za Taifa, hivyo tayari ameagiza viongozi wa ngazi za kata na vijiji kupeleka matangazo kwa wafugaji juu ya kitakachofanyika siku chache zijazo.

“Tayari tumewapa taarifa za kuwataka waondoke wenyewe kandokando ya hifadhi na hasa wale waliovamia maeneo ambayo yanatumiwa na wanyama kama mazalia yao.

“Tumegundua pia kwamba, wafugaji hao nyakati za usiku wanalisha mifugo ndani kabisa ya hifadhi, sasa jambo hilo hatuwezi kulikubali, lazima tuwaondoe na kuwafikisha mahakamani.

“Kwa kifupi, wafugaji hao wanaharibu mazingira kwa kukata miti wanayoitumia kujenga maboma yao ndani ya hifadhi ya Serengeti, jambo ambalo nalo hatuwezi kukubali liendelee kuwapo,” alisema Mtaka.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete, alisema kitendo cha wafugaji hao kuvamia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni kati ya maajabu saba ya dunia, haikubaliki na mifugo yote itakayokamatwa itataifishwa.

“Kulisha mifugo katika hifadhi ya Taifa ni kinyume na sheria na sheria inatutaka kupiga faini au kutaifisha mifugo itakayokamatwa ndani ya hifadhi,” alisema Shelutete.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles