DK. SHEIN AHIMIZA UMAKINI MIKATABA YA MADINI

0
820
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjukuu wake Ali Abdalla Mitawi katika Kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.Picha na Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjukuu wake Ali Abdalla Mitawi katika Kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.Picha na Ikulu.

Na MWANDIDHI WETU- ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuna haja kwa Serikali kuwa makini wakati wa kuandaa, kusimamia na kufuatilia mikataba ya mafuta na gesi.

Dk. Shein aliyasema hayo jana katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd El Fitri lililofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi, Kikwajuni, mjini Zanzibar.

“Mikataba ya mafuta na gesi asilia isiwanufaishe watu wachache na makampuni yao kwa njia za kijanja.

“Nasema hivyo kwa sababu baada ya kukamilika kwa kazi ya kutunga sheria ya mafuta na gesi asilia, kinachotakiwa sasa  ni kuandaa mikataba ya mafuta na gesi asilia.

“Uongozi wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kwa kushirikiana na wataalamu na taasisi zote zinazohusika katika kuandaa mikataba hiyo, wafahamu kuwa rasilimali hizo ni za Wazanzibari wote na hivyo lazima wawe makini wakati wote.

“Kwa maana hiyo, kila mmoja anatakiwa ajue  ana dhamana na jukumu kubwa la kuhakikisha masilahi ya Zanzibar na wananchi wake yanalindwa na vigezo vyote muhimu vinazingatiwa,” alisema Dk. Shein.

Wakati huo huo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa juhudi anazoendelea kuzichukua katika kukuza uchumi, ikiwamo ufufuaji na uendelezaji wa sekta ya viwanda na uzuiaji wa usafirishaji wa mchanga wenye dhahabu nje ya nchi.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka Watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, wamuunge mkono Rais Dk. Magufuli ili aendelee kufanya mambo mema zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here