25 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

OFISI ZA UMMA ZIJALI TOVUTI ZAO

NA SHERMARX NGAHEMERA

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, wiki jana alizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na tovuti mpya ya kituo hicho kitu ambacho kiliwashangaza wengi juu ya mapungufu ya wazi ya taasisi hiyo nyeti kwa uchumi wa Tanzania.

Wakati kuzindua bodi ni kawaida lakini uzinduzi wa tovuti ulikera wengi kwani inaonekana bila kuingia Geofrey Mwambe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kwa miezi minne tu hadi sasa ameona mapungufu haya makubwa kwa ustawi wa taasisi hiyo na Tanzania kwa ujumla na kudai mabadiliko ya msingi. Ninampongeza kwa hili.

Rais Dk. John Magufuli amemteua Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Profesa Longinus Rutasitara, badala ya Profesa Lucian Msambichaka aliyemaliza muda wake jambo ambalo ni la kawaida katika utawala wa vyombo vya umma.

Lakini Uzinduzi wa tovuti mpya ulishitua watu kwani walishindwa kuelewa taasisi nyeti kwa uchumi kukosa mawasiliano na umma kwa ujumla kupitia tovuti na haswa maelezo yalipotolewa kuwa tovuti iliyokuwepo nayo ilikuwa inamilikuwa sio na Tanzania Investment Centre (TIC) bali na kampuni binafsi iliyoko nje ya nchi; wao ndio waliokuwa wanaamua yote ya tovuti hiyo yaani kusuka au kunyoa kuhusu nchi yetu.

Uzinduzi huo ulilenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa TIC na kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kuhusiana na fursa za uwekezaji na utalii nchini mwetu. Tovuti inapunguza gharama kwa wenye nia ya kuwekeza nchini kupata taarifa za awali kuhusu mazingira, ya uwekezaji.

Taarifa  sahihi za nchi  kama miundombinu, maeneo ya uwekezaji, aina ya miradi inayoweza kupata msamaha wa kodi na vigezo vyake, upatikanaji wa nishati, maji na ardhi yenyewe kimsingi viliminywa au kupatikana kwa shida. Hatuwezi kukataa kuwa hujuma haikufanyika ili kupunguza kasi ya kukua uchumi wetu.

Ndio maana lawama zilitoka kila upande wa dunia zikidai ugumu  wa kufanya Biashara Tanzania . Kiwango chetu kilishuka na tukawa ni wa nchi ya 152 toka nafasi ya 98 ya awali pamoja kuwa na rasilimali nyingi.

Mwambe anasema tovuti hiyo itakuwa chachu katika utoaji wa taarifa zinazohusu fursa na huduma za uwekezaji na mazingira ya uwekezaji nchini. Tunampa hongera nyingi Mkurugenzi huyo.

TIC ilikuwa na mapungufu makubwa katika tovuti yake ambayo uendeshaji wake haukuwa chini yake hata yeye ilimshangaza.

Hivi basi tunaomba ofisi zote za umma zijitatiti kwa wakati huu kumiliki, kuziendesha na kuzidhibiti tovuti zao kwani tovuti sio sayansi ya roketi ya kwenda Mars. Kila mtu anaweza kumiliki na kuendesha tovuti na ninaomba kosa hilo lisirudiwe popote kwenye ofisi ya umma.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles