25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Republican yalipuliwa kwa  bomu Marekani

Hillary ClintonWASHINGTON, MAREKANI

OFISI   ya Chama cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto baada ya kitu kinachodhaniwa kuwa bomu lililotengenezwa kienyeji kurushwa ndani ya ofisi hiyo huku jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama hicho.

Chama hicho kimesema chupa iliyojazwa mafuta yanayoweza kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha Republican iliyoko eneo la Orange.

Mkurugenzi wa   Republican, Dallas Woodhouse, alisema  hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba tahadhari ya usalama imetumwa katika ofisi nyingine za chama hicho.

”Wanachama wa Nazi walio katika chama cha Republican ni sharti waondoke mjini,” alitahadharisha Woodhouse.

Mgombea Urais wa Cmama cha Democrat, Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba shambulio hilo ni ”la kutisha na halikubaliki.”

Mgombea Urais  wa Chama cha Republican, Donald Trump, alionekana akiwalaumu wafuasi wa   Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.

”Wanyama wanaomwakilisha Hillary Clinton huko North Carolina walirusha bomu katika ofisi yetu ya   Orange kwa sababu wanajua tutashinda,” alisema Trump katika mtandao wake wa Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles