Ofisa  China kunyongwa kwa  kuficha fedha nyumbani

0
636

wei-pengyuan-950x550

BEIJING, CHINA

OFISA wa zamani wa ngazi ya juu   China, Wei Pengyuan, yupo hatarini kuhukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya  kuficha dola za Marekani milioni 30 nyumbani kwake. Hukumu yake imeahirishwa.

Wei Pengyuan alikuwa ofisa mkuu aliyesimamia biashara ya makaa ya mawe   China.

Mahakama mjini Baoding, kaskazini mwa China, imesema  Wei alipokea rushwa alipokuwa akiidhinisha miradi ya makaa ya mawe.

Maofisa wa serikali walisema mashine nne za kuhesabu fedha ziliharibika walipokuwa wanajaribu kuhesabu fedha zilizopatikana nyumbani kwa ofisa huyo.

Maelfu ya maofisa wa serikali wameadhibiwa katika  kampeni kubwa ya kukabiliana na ulaji rushwa   China.

Kampeni hiyo ambayo inaungwa mkono na Rais Xi Jinping imesababisha  kuadhibishwa kwa baadhi ya wapinzani wa  siasa wa Rais Xi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here