WALIOKUWA washiriki wa Shindano la Bongo Star Search 2015 wameteuliwa kuwa mabalozi wa kampeni ya ‘Jiekotishe na Huawei’ sambamba na uzinduzi wa simu mpya maalumu kwa msimu wa sikukuu.
Mabalozi hao ni Nassib Fonabo aliyeshika nafasi ya pili katika shindano la BSS, Frida Amani mshindi wa tatu na Kelvin Gerrison.
Naye Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Samson Majwala, alisema wamezindua kampeni hiyo kwa lengo la kutoa zawadi kwa watakaonunua simu hizo.