Aneth Kushaba kufungua mwaka na ‘Call Me’

0
1107

KushabaNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII na Mkurugenzi wa Bendi ya Stars, Aneth Kushaba, amesema anatarajia kuvunja ukimya wake mapema mwakani na wimbo unaoitwa ‘Call Me’ ambao ameufanya kwenye studio za B Hits chini ya mtayarishaji, Pancho Latino.

Aneth alisema kwa muda mrefu amefanya kazi chini ya bendi hivyo mashabiki wake wamekuwa wakiuliza kazi zake binafsi zitatoka lini na ameamua kuwajibu kwa kuutoa wimbo huo utakaotoka Januari mwakani.

“Huo ni wimbo wangu binafsi, kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya kazi za bendi lakini mapema Januari mwakani nitaachia wimbo wangu audio na video na hizi zitakuwa ni kazi endelevu kwangu,” alisema Aneth.

Aliongeza kuwa majukumu aliyonayo kwenye bendi yake hayataathiri mfululizo wa kutoa kazi zake binafsi kwa kuwa hivi sasa amejipanga kurudi kwenye muziki kwa kishindo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here