Kardashian ahofia kupata kisukari

0
728

kim-kardashianNEW YORK, MAREKANI

MKE wa Kanye West, Kim Kardashian, amehofia kupata ugonjwa wa kisukari kutokana na ulaji wake wa ovyo wa vyakula vya aina mbalimbali kipindi hiki cha ujauzito wake.

Mrembo huyo anatarajia kupata mtoto wa pili kabla ya Desemba 26.

“Ninaamini nina afya njema, lakini kuna wakati najikuta nakula bila mpangilio hivyo naweza kupata ugonjwa wa sukari, ninaamini hali hii inatokana na ujauzito na ndiyo maana muda mwingi natamani kula,” alisema Kim.

Hata hivyo, mrembo huyo atakuwa na furaha kubwa ya kuongeza familia yake hivi karibuni. “Familia inatarajia kuwa kubwa muda mfupi ujao, kwa sasa tupo watatu, lakini hadi kufika Desemba 27 tutakuwa na familia ya watu wanne,” aliongeza Kim.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here