24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Nyavu Simba, Yanga hazitawasahau nyota hawa

ZAINAB IDDY

WATAALAMU wa mambo ya mahusiano wanaeleza kuwa, baada ya wanandoa kupeana talaka, hakuna kitu kinaweza kumuumiza mmoja wao kama kumuona mwenzake akionekana kufurahia maisha na mke, mume mpya.

Wakati mwingine hali hii inatokea hata katika maisha ya soka. Ni pale mchezaji anapotoka timu moja kwenda timu nyingine, kisha kusababisha kilio kule kwa waajiri wake wa zamani.

SPOTIKIKI wiki hii inakuletea nyota waliokipiga katika klabu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti na kuweka rekodi ya kufunga mabao katika michezo ya timu hizo wakiwa na vikosi vyote viwili.

Amiss Tambwe

Alitambulika katika soka la Tanzania msimu wa 2013/14, akiletwa Tanzania kutoka nchini Burundi na Simba.

Katika msimu huo, Tambwe aliweza kuibuka mfungaji bora akiwa na mabao 17, kati ya hayo, moja aliifunga Yanga katika mechi ya watani wa jadi ya ligi.

Tambwe ameingia katika orodha ya kuzifunga Simba na Yanga ambazo zote amezichezea katika msimu wa 2014/15 mechi ya lala salama baada ya kuachwa na Wekundu wa msimbazi dakika chache kabla ya dirisha la usajili mdogo kufungwa na Jangwani kumsajili.

Kwa sasa Tambwe yupo nchini kwao Burundi, alindoka Tanzania akiwa na rekodi ya kipekee ya kufunga mabao 4 katika mechi za watani wa jadi, ambapo moja akiifunga Yanga akiwa Simba na matatu aliziona nyavu za Simba akiwa Yanga.

Emmanuel Okwi

Kwa mara ya kwanza alitua ardhi ya Tanzania, msimu wa 2008/09 aliposajiliwa na Simba akitokea SC Villa ya nchini kwao Uganda.

Okwi alianza kufunga kwenye mechi ya watani, wakati Simba ilipoichapa Yanga mabao 5-0, mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Mei 6, 2012, Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo, Okwi alifunga mabao mawili, huku mengine yakiweka kimiani kwa mikwaju ya penalti na kipa Juma Kaseja, Felix Sunzu na marehemu Patrick Mafisango.

Baada ya kuonyesha ubora Simba msimu wa 2013/14, Okwi aliihama Simba na kujiunga na mahasimu wao Yanga.

Desemba 21, 2013,alicheza mechi ya watani wajadi mchezo wake wa kwanza wa watani, ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Okwi.

Huo ulikuwa mchezo maalum uliopewa jina la ‘Nani Mtani Jembe’.

Bao hilo lilimfanya Okwi kuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga mabao katika mechi ya watani kwa wakicheza timu zote mbili.

Athuman China

Mashabiki wa soka walikuwa wakimfananisha naSalvatory Edward ‘Dokta’ kiuchezaji wake, ingawa China alisifika zaidi kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira na kutoa pasi zilizonyooka.

Nyota huyo alianza kucheza soka la ushindani miaka ya 90 akiwa na Yanga waliomsajili, baada ya kumuona akifanya vizuri katika timu ya Printpak, iliyokuwa ikimilikiwa na kiwanda cha kuchapisha magazeti.

Akiwa ndani ya uzi wa kijani na njano, aliifunga Simba katika mchezo wa ‘derby’ msimu wa 1990/91 pale Yanga iliposhinda mabao 2-1. 

China aling’ara Yanga hata kupata nafasi  ndani ya timu ya Taifa kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa Uingereza lakini hakuweza kuimili changamoto  kule alikokwenda 

Baada ya kusambaa kwa taarifa za kurejea kwake, Azim Dewij ambaye alikuwa mfadhiri wa Simba enzi hizo alimsainisha na akawa mcheza Wekundu wa msimbazi alikoweza kuifunga Yanga pia katika mechi ya Watani msimu wa 1994/95 mechi ikiisha kwa sare ya 1-1.

Thomas Kipese ‘Uncle Tom’

Mwishoni mwa mwaka 1992 timu za Simba na Yanga ziliingia katika mzozo mkubwa kila mmoja akidai kumsajili winga hatari Kipesa wengi wakimuita ‘Uncle Tom’.

Katika mzozo huo, Simba ilishinda vita na kumsajili Kipese huku Yanga waliomuibua mwaka 1990 kutoka Printpak FC wakiambulia patupu.

Akiwa na Yanga msimu wa 1990/91 Ancle Tom aliwafunga Simba bao 1- katika ushindi wa 2-1  kisha kafany hivyo tena msimu wa 1991/92 mechi ya mzunguko wa pili pale Simba iliposhinda 2-1  huku  Ancle Tom akiipa bao pekee Yanga.

Kitendo cha kuwafunga mara mbili mfululizo kilionekana kuwauma Simba waliopambana kuhakikisha wanamshawishi kwa dau kubwa hadi kusaini kwao msimu wa 1992/93 ambako aliweza kuwafunga waajiri wake wa zamani katika derby mechi ikiisha kwa ushindi wa 3-2.

Said Mwamba ‘Kizota’

Ni miongoni mwa nyota waliocheza timu za Simba na Yanga na kuweka rekodi ya kuzifunga zote.

Kizota ambaye alijiunga na Yanga alijiunga na Yanga mwaka 1986 na mechi yake kuwatumikia Wanajangwani ilikuwa dhidi ya CDA ya Dodoma iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika msimu wa 1989/90, Kizota aliifunga Simba, katika mchezo wa wapinzani iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Mwaka 1995 , Simba ilipanda dau na kumuwekea fungu kubwa lililomshawishi kumwaga wino,ndipo alipofanikiwa kuwafunga waajiri wake wa zamani katika mchezo uliomalizika kwa Wekundu wa Msimbazi kushinda 1-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles