23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Njia 10 ambazo ugonjwa wa corona unavyosumbua

RIO de Jeneiro,Brazil

SHIRIKA la Utangazaji la Uingereza (BBC), limeorodhesha maambukizi ya virusi vipya vya corona kuwa janga au  na suala nyeti.

Ndani ya miezi miwili, virusi hivyo vimesambaa hadi mabara kadhaa, ikiwamo kusambaa kwa kasi ya hali ya  juu kwa zaidi ya mabara matatu.

Huenda tayari tumefikia awamu hiyo ,

Kwa mara ya kwanza katika historia tunakabiliwa na janga hatari, vyombo vyote vya habari kila siku duniani vinazungumzia ugonjwa huo.

Taarifa zinasema nchini Brazil,virusi hivyo vimezaana mara tatu zaidi.

Kutokana na hali hiyo, kuna mambo 10 mapya kuhusu ugonjwa hup

1.Tunafahamu ni ugonjwa gani

Kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ukimwi kilitangazwa Juni, 1981 na ilichukua zaidi ya miaka miwili kugundua virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Visa vya kwanza vya ugonjwa hatari wa mapafu viliripotiwa nchini China, Desemba 31, mwaka jana na ilipofikia Januari 7, mwaka huu, virusi hivyo tayari vilikuwa vimefichuliwa. Virusi vya Corona viligunduliwa siku 10 baadaye.

Tayari tunajua ni virusi vipya kutoka familia moja na virusi vya SARS . Ugonjwa huo umepatiwa jina COVID19. Unahusishwa na virusi vya corona kutoka kwa popo.

2. Tunajua jinsi ya kuvigundua 

Sampuli ya RT-PCR inapatikana kila mahali tangu  Januari 13, mwaka huu. Katika miezi ya hivi karibuni vipimo hivyo vimeboreshwa .

3. China hali inaimarika

Udhibiti mkali na mikakati ya kuwatenga walioambukizwa imeanza kuzaa matunda.

Kwa wiki kadhaa sasa idadi ya watu wanaopatikana na virusi hivyo imepungua kila siku. Katika mataifa mengine , visa vya maambukizi vinafuatiliwa kwa kina .

Mikakati iliowekwa, ni ya nguvu na visa vinaweza kudhibitiwa kwa urahisi kwa mfano nchini Korea kusini na Singapore.

4. Asilimia 80 havijaonyesha makali

Ugonjwa huo hautoi ishara ama hauna makali kati ya visa asilimia 81.

Katika asilimia 14 iliosalia vinaweza kusababisha ugonjwa hatari wa mapafu na asilimia tano vikiwa hatari na hata kusababisha kifo

5. Watu wanapona

Data ya pekee ambayo inaonyeshwa na vyombo vya habari, ni ongezeko la visa vilivyothibitishwa na idadi ya vifo.

Lakini idadi kubwa ya watu walioambukizwa wamepona. Idadi ya watu waliopona ni mara 13 zaidi ya waliofariki na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

6. Virusi  haviwaathiri watoto 

Ni asilimia tatu pekee ya watu walio chini ya umri wa miaka 20 walioathirika na idadi ya vifo ni asilimia 0.2. kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40.

Miongoni mwa watoto dalili, ni chache hali ya kwamba mara nyengine hazionekani.

7. Ni rahisi kuua virusi

Virus hivyo vinaweza kuuliwa katika sakafu kupitia ethanol , Hydrogen peroxide au sodium hypochlorite katika dakika moja pekee.

Uoshaji wa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni, ndiyo njia bora ya pekee ya kuzuia maambukizi.

8. Ripoti 150 za kisayansi.

Ni wakati wa sayansi na ushirikiano. Katika kipindi cha mwezi mmoja , takriban ripoti 164 zimeandikwa kuhusu ugonjwa COVID19 au SARSCov2, ikiwemo ripoti nyengine nyingi zaidi ambazo hazijachapishwa.

Ni kazi za ya utangulizi juu ya chanjo, matibabu, ugonjwa, jeni na phylogeny, utambuzi na mambo ya kliniki.

Ripoti hizo zinaandaliwa na watunzi kote duniani.

Mwaka 2003, wakati virusi vya SARS vilipotokea , ilichukua zaidi ya mwaka mmoja kupata chini ya nusu ya ripoti kama hizo.

Majarida mengi ya kisayansi yameweka wazi ufadhili wao wa virusi vya corona.

9. Sampuli tofauti 

Uwezo wa kutafuta chanjo tofauti ni mzuri. Tayari kuna zaidi ya miradi minane dhidi ya virusi hivyo.

Makundi yalioanzisha juhudi za kutafuta chanjo dhidi ya virusi vingine kama hivyo.

Kile kinachorefusha uboreshaji wake ni vipimo vyote muhimu vya sumu yake, madhara yake , usalama wake , kinga na uwezo wake katika kinga.

Haki miliki ya picha Getty Images

10. Kuna majaribio 80

Chanjo zina kinga. Umuhimu wake zaidi ni tiba ya watu ambao tayari ni wagonjwa. Tayari kuna majaribio 80 ya kutafuta tiba ya virusi vya corona.

Hizi ni dawa ambazo zimetumika kwa mambukizi mingine ambayo tayari yamethibitishwa na tunajua ziko salama.

Mojawapo ya dawa hizo ambayo tayari imejaribiwa katika binadamu ni dawa ya remdesivir – dawa ya virusi vya ukimwi ambayo bado inafanyiwa utafiti ambayo imejaribiwa dhidi ya magonjwa kama vile Ebola na SARS/MERS.

Dawa nyingine ni ile aina ya Chloroquine, dawa ya kukabiliana na malaria ambayo

pia ina uwezo wa kukabiliana na virusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles