Baba Kanumba afariki Dunia

0
873

MWANDISHI WETU – SHINYANGA

BABA mzazi wa mwigizaji nyota nchini, Steven Kanumba, Charles Kanumba, amefariki Dunia jana asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa maradhi ya presha na maumivu ya nyonga.

Mdogo wake Kanumba anayeitwa Mjanaeli, ameliambia MTANZANIA kuwa mzee wao alikuwa anaumwa muda mrefu na alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga alipokuwa anapatiwa matibabu mpaka alipofariki Dunia.

“Baba yetu mzee Charles amefariki saa nne leo (jana) asubuhi hapa, Hospitali ya Mkoa, kwasasa tunaendelea na taratibu zingine na tutaendelea kutoa ratiba ya mazishi kikao cha familia kukaa,” alisema Mjanaeli.

Hivi karibuni baba Kanumba aliibuka na kuomba kugawana nusu kwa nusu na mama Kanumba malipo ya awamu ya pili yatakayotolewa na moja ya kampuni alizowahi kufanya nazo kazi Steven Kanumba enzi za uhai wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here