24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

NYALANDU AJIUZULU UBUNGE, AOMBA KUHAMIA CHADEMA

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameomba kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kujiuzulu ubunge wa jimbo hilo na kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Kwa mujibu wa Nyalandu ambaye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, amejiridhisha kuwa mwenendo wa hali ya kisiasa  na kiuongozi na kiuchumi iliyopo sasa nchini, chama hicho kimepoteza mwelekeo wake.

“Aidha naamini kuwa kama ilivyokuwa kwa mihimili mingine kuingiliwa na serikali kwa namna moja au nyingine ccm nayo imekuwa chini ya miguu ya dola  badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa serikali  inapobidi kama ilivyokuwa maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Hivyo basi, kwa dhamira na uamuzi wangu mwenyewe nikiwa na haki ya kikatiba, natangaza rasmi kukihama CCM na nitaomba ikiwapendeza wanachama Chadema waniruhusu kuingia malangoni mwao ili kuleta maendeleo ya kidemokrasia nchini.

“Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa naadhi ya Watanzania wenzangu na kutokuwapo kwa mipaka ya wazi ya mihimili ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Tunapofanya utendaji wa kazi wa kutunga sheria na kusimamia kutokuwa na uhuru ulioainishwa na kuwekwa bayana kikatiba,” amesema Nyalandu.

Pamoja na mambo mengine, Nyalandu amesema bila Tanzania kupata Katiba Mpya kwa sasa hakuna namna ya kufanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwapo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa mihimili hiyo ambayo ndiyo chimbuko na uongozi bora wa nchi na kuonyesha kwa wazi kuwa madaraka yote yanatokana na wananchi wenyewe na kwamba serikali ni sharti iwe ya watu kwa ajili ya watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles