24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yamwaga vifaa vya shule Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wilaya za Chamwino na Dodoma. mjini zimepokea madawati na meza kwa shule za msingi na Sekondari kutoka Benki NMB ili kupunguza uhaba uliokuwepo.

NMB ilikabidhi kwa shule hizo jumla ya madawati 450, Viti 60 na meza 60 ambavyo nina thamani ya Milioni 53 kwa ujumla wake huku ikiahidi kushirikiana zaidi na Taasisi zingine.

Madawati yaliyotolewa na benki hiyo yalielekezwa katika shule za msingi Dabalo, chiwondo, Igamba na Msanga, Buigiri na Makang’wa pamoja na hospitali ya kwa wilaya ya Chamwino wakati Dodoma mjini Shule za Msingi Mazengo, Chadulu na Solou zilinufaika.

Akikabidhi vifaa hivyo, Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mulozi alisema msaada huo ni sehemu ya faida ambayo benki hiyo hurudisha kwa wananchi katika miradi ya maendeleo.

Mlozi alisema NMB imetenga Sh bilioni 1 kwa ajili ya miradi kwa wananchi ambayo inatokana na faida waliyoipata mwaka jana kutokana na Watanzania kuwekeza fedha zao kwa benki hiyo.

“Tunayo maeneo manne tunayoweza kuhudumia ambayo ni eneo la elimu, afya, majanga na elimu ya fedha, kwa hiyo tunafanya kadri tuwezavyo ili kuwarudishia wananchi kwa ajili ya maendeleo kwenye sekta hizo,” alisema Mulozi.

Meneja huyo aliwaomba Watanzania kutumia benki ya NMB kwa ajili ya kuhifadhi fedha zao kwani ni benki salama inayowajali wanyonge kwa kuwarudishia maendeleo hadi kwenye maeneo yao.
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe alisema michango ya benki hiyo imesaidia kupunguza uhaba wa madawati unaoikabili wilaya kwa sasa.

Profesa Mwamfupe alisema alisema NMB imekuwa msaada na kimbilio katika miradi mingi inayotekelezwa katika Jiji la Dodoma ambalo limekuwa na upungufu mkubwa wa madawati kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari.

Meya alisema ni wakati wa Watanzania kuamka na kuanza kuitumia benki ya NMB kwa kila namna ikiwemo kuwafundisha watoto jinsi ya kuitambua benki hiyo na akaonyesha mfano kwa kuwafungulia akaunti zaidi ya watoto 10.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde alisema benki hiyo imekuwa msaada na rafiki wa karibu katika Maendeleo ya Jimbo hilo ambapo miradi mingi imekuwa na mkono wa NMB.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles