29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri zatakiwa kutunza Malikale

Na Sheila Katikula, Mwanza

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafanya kazi kwa ushirikiano na Wizara ili waweze kutambua maeneo ya malikale sanjari na kuyaendeleza, kuyatangaza kama vivutio vya utalii ili kuleta manufaa na fursa kwenye sekta ya utalii.

Nduhiye alitoa wito huo  jana wakati wa kikao cha wadau cha wa sekta ya utalii kulenga kujadili utekelezaji wa sera ya malikale ya mwaka 2008 kilichowakutanisha  wadau wa malikale mkoani hapa.

Alisema halmashauri ni wadau muhimu  wa kutangaza na kuendeleza vivutio hivyo ni lazima zitambue nafasi za malikale kwani wanayo nafasi kubwa kuhamasisha utalii wa ndani na wa nje kwa kutumia maeneo yao yenye vivutio.

Alisema  serikali za mitaa, taasisi za umma na watu binafsi kwa pamoja wanatakiwa kushiriki kuhifadhi na kuendeleza malikale  zilizopo kwa manufaa ya sasa na baadaye kwani wizara ipo tayari kusaidia kuyatangaza maeneo hayo yaliyopo ili yahifadhiwe na kulindwa  kwa mujibu wa sheria.

Alisema Wizara haina wataalamu wa malikale  katika ngazi ya Serikali  za mitaa lakini inawaamini  maafisa utamaduni  waliopo kwenye ngazi tofauti ambao wanaweza kutumika katika uhifadhi na uendelezaji wa malikale  zilizopo.

Alisema  maeneo ya malikale  yaliyotangazwa kwenye  gazeti la serikali ni 131  ambapo  kati ya hayo  yanayohifadhiwa na serikali  kuu  na kuwekewa miundombinu  ni 18 sawa na asilimia 60 na maeneo  yaliyobaki   yanamilikiwa na watu binafsi na taasisi za umma.

Aliongeza, kwa mujibu wa sera ya malikale ya mwaka 2008 na sheria ya sura ya 333 kifungu cha 16 kinaelekeza serikali za mitaa  kutunga  sheria ndogo ndogo kwa ajili ya  kuhifadhi ,kulinda na kuendekeza vivutio  vilivyopo kwenye maeneo hayo ili kuendeleza historia na urithi wa taifa.  

Naye Kamishina  Msaidizi  wa  Uhifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya kisiwa Cha SaaNane, Eva Mallay alisema kutokana na kikao hicho cha wadau cha kuzitambulisha malikale na malikale kitasaidia kuongeza vivutio vya utalii.

Alisema watalii  wanapokuja mkoani hapa watapata fursa ya kukaa muda mrefu kujifunza na kutembelea vivutio vilivyopo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kwani watu walikuwa hawatambui kama kuna malikale  za aina vyingi  ambazo  zikitembelewa zitapelekea kukuza utalii  na kuongezea pato la taifa.

Kwa upande wake Msimamizi wa ofisi ya bodi ya utalii Tanzania Kanda ya ziwa,Gloria Munhambo aliwashukru waandaaji wa kikao hicho kwani mipango waliyoweka itasaidia kuongeza idadi ya watalii kuona na kujifunza mambo ya kale na makumbusho  ya historia ya kabila la Wasukuma Bujora.

“Tunataka kuongeza  mazao ya utalii, utalii siyo wanyama tu, kutembelea fukwe ,miamba na mawe  lakini kuna mambo ya kale na makumbusho kwa mfano  mkoani Mwanza kuna makumbusho ya historian ukienda pale utajifunza mambo mengi na vifaa vya asili nabkupelekea kuvitangaza,” alisema Munhambo.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dk. Noel Lwoga alisema kazi zao kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1980 ni kuhakikisha wanakusanya, kuhifadhi mikusanyo ya asili, utamaduni, kutoa elimu kwa jamii kuhusu urithi wa taifa kusimamia malikale 91 nchi nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles