25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Niyonzima alonga kuelekea mechi dhidi ya Simba

NA WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM

KIUNGO fundi, Haruna Niyonzima, amewasili jijini Dar es Salaam jana tayari kuitumikia timu yake mpya ya Yanga, akitokea AS Kigali ya nchini kwao, Rwanda.

Niyonzima amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea AS Kigali, ikiwa ni baada ya kutemwa na Simba waliomng’oa Jangwani misimu mitatu iliyopita.

Niyonzima ametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana, ikiwa ni saa chache kabla ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga litakalopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini.

Akizungumza baada ya kutua nchini, Niyonzima alisema yupo tayari kabisa kuitumikia Yanga kwa uwezo wake wote, japo alitamani kupangwa hata katika pambano la kesho ambalo si geni kwake.

Haruna Niyonzima

“Nimefurahi sana kurudi Tanzania kwa ajili ya kuanza kuitumikia Yanga, Yanga kwangu ni kama nyumbani kwani nimekuwa nao kwa muda mrefu na ndio walionifanya nijulikane zaidi.

“Binafsi nipo fiti na nipo tayari kucheza hata leo, ingewezekana hata mechi ya Jumamosi ningekuwa tayari kucheza…mashabiki na wachezaji wa Yanga naomba wanipokee na kunipa ushirikiano,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli ‘HB’, alisema wao wameshakamilisha usajili wa mchezaji huyo hivyo jukumu la lini ataanza kuichezea timu yao, wanaliacha kwa kocha wao, Charles Mkwasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles