26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Nicki Minaj amuanika mtoto wake

NEW YORK, MAREKANI 

HATIMAYE msanii wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, amemuanika mtoto wake kwa mara ya kwanza tangu alipojifungua mwishoni mwa mwezi uliopita.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 37, alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuposti picha ya mguu wa mtoto huyo wa kiume huku akimtakia heri mume wake Kenneth Petty.

“Nakutakia siku njema mume wangu, nakupenda sana na mini ndio mke wako na mama wa mtoto wako,” aliandika msanii huyo chini ya picha hiyo.

Hiyo ni picha ya kwanza ya mtoto wa Nicki Minaj kuonekana machoni mwa watu, lakini mashabiki walionekana bado wanatamani kuiona hata sura ya mtoto huyo.

Mrembo huyo amekuwa msiri kwenye masuala ya familia, hata alipokuwa mjamzito alitoa picha moja ya ujauzito wake hadi anajifungua tofauti na ilivyo kwa mastaa wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles