27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Trump na Obama warushiana vijembe wakati wa mkutano wa kampeni

Washington, Marekani 

RAIS Mstaafu wa Marekani Barack Obama, ambaye anampigia chapuo mgombea wa Democratics Joe Biden anayewania urais wa Marakani, amempiga kijembe Rais Donald Trump akimuhusisha na mjomba aliyechanganyikiwa.

Wakati Obama akisema hayo huko Pennsylvania, Trump aliyekuwa North Carolina, anayewania muhula wa pili kupitia chama cha Republican, alimkebehi Obama kwa kukosea katika uchaguzi wa mwaka 2016 .

Huku siku 13 zikiwa zimesalia kufikia siku ya uchaguzi, Biden anaonekana bado anaongoza katika kura za maoni.

Lakini ni kiwango kidogo sana kwa mapendekezo hayo kuwa uhalisia, matokeo ya kuamua nani atakuwa rais yatajulikana Novemba 03.

Wamarekani wengi wanaonekana kuwa wanapiga kura ya maoni kwa wingi mwaka huu, mpaka sasa tayari kura milioni 42 za maoni zimepigwa.

Trump alisema nini?

Katika kampeni zake Trump alimshambulia mpinzani wake wakati wote.

Alisema ni maamuzi ya wapiga kura kuchagua kati ya “Trump ili wapone kabisa ” au “Biden waingie kwenye msongo wa mawazo”.

Biden alipumzika wiki nzima kwa ajili ya kujiandaa na mjadala wa mwisho wa marais utakaofanyika usiku wa Alhamisi huko Nashville, Tennessee, wakati Trump akiwa anaendelea na kampeni katika majimbo ya pembezoni.

Rais hakusita kuingilia kati kampeni aliyoifanya Obama, kwa mara ya kwanza tangu kampeni hizo zianze mwezi Agosti.

“Hakukua na mtu yeyote ambaye alifanya kampeni kubwa kama Hillary Clinton zaidi ya Obama, si ndio?” Trump aliwaambia walioshiriki mkutano huo, alikuwa kila mahali.

Rais aliongeza: “Nadhani mtu ambaye hakuwa na furaha wakati Hillary aliposhindwa alikuwa Barack Hussein Obama.”

Trump alimkejeli tena Obama kusema kuwa Biden hakuwa na vigezo vya kuwa rais, alipokua makamu wa rais mwaka 2009-2017.

Mwaka 2016, Obama aliripotiwa kuwa alimweka kando Biden kuwania nafasi ya urais na kumpa nafasi Hillary Clinton akiamini kuwa alikuwa anaweza kumshinda Trump.

Mwaka jana Obama alisema kuna uhitaji wa kuwa na mtu mpya katika uongozi wa Democratic, taarifa ambayo ilitafsiriwa kuwa hamkubali Biden.

Obama alisema nini? 

Baada ya kumshambulia Trump namna alivyokabiliana na virusi vya corona na uchumi, Obama aligeukia mkutano wa Philadelphia kuhusu ujumbe wa Twitter wa rais.

Alisema ikiwa Biden atashinda, “hatutakuwa na rais ambaye anatukana yeyote asiyemuunga mkono, au kutishia wengine kwa kuwapeleka gerezani. Hiyo sio tabia ya kawaida kwa rais”.

Obama ambaye bado ni miongoni mwa watu mashuhuri katika chama cha Democratic  alisema wapiga kura hawatavumilia tabia kama hizo kutoka kwa mmoja wa familia yao, “isipokuwa pengine kwa mtu asiyekuwa na akili timamu kwengineko”.

“Kwanini watu wanatafuta visingizo kwa hilo?” alisema. “Oh, huyo ni yeye tu. Hapana! 

“Wanahamasisha wengine kuwa wakatili. Na kugawanya watu. Na kuendeleza ubaguzi. Na huko kunaharibu jamii yetu.”

Aliongeza: “Tabia ni muhimu. Sifa ya mtu ni muhimu pia.”

Kuhusu janga la corona, Obama alizungumzia hatua za hivi karibuni za Trump kuhusu Covid-19: “Donald Trump hawezi kutulinda sisi. Yeye mwenyewe. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles