26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Wakili mbaroni kwa shtaka la kujeruhi kwa makusudi

NA GODFREY SHAURI, DAR ES SALAAM

Wakili Jackline Ghikas (24), Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika ya Mahakama ya Wilaya ya Hakimu mkazi Kinondoni kwa shtaka la kujeruhi kwa makusudi.

Awali akisoma hati mashtaka mbele ya Hakimu  Franco Kiswaga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sylha Mitanto, alidai Septemba 9 mwaka jana, katika eneo la Mbezi Beach, mshitakiwa alimpiga na kumjeruhi kwa makusudi  Timotheo Jeremiah.

Hata hivyo mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo mbele ya Hakimu Kiswaga huku upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Hakimu Kiswaga alisema kesi hiyo inadhaminika endapo mshtakiwa atakidhi vigezo vya dhamana vya kuwa na mdhamini mmoja  atakaye saini bondi ya Sh milioni mbili   au pesa taslimu.

Alisema mdhamini huyo anatakiwa kuwa mwaaminifu, mfanyakazi wa Serikali au taasisi binafsi inayo tambulika Serikalini na mwenye barua kutoka Serikali ya Mtaa.

 Mshtakiwa alirudishwa rumande baada ya mdhamini wake kuwa na barua kutoka Serikali za Mtaa lakini hakusaini bondi ya Sh milioni mbili na shauri hilo litatajwa tena Novemba 11 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles