27 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

NGOME YA MBOWE YATIKISWA TENA

Na MWANDISHI WETU – HAI


NI mwendelezo wa mtikisiko wa kisiasa ndani ya Jimbo la Hai ambalo linaongozwa na  Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe,  baada ya Diwani wa Kata ya Romu, Shilimiafoo Kimaro kujiuzulu kiti chake jana na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Kimaro anakuwa diwani wa sita kupitia Chadema kuchukua uamuzi kung’atuka katika kiti chake na kujiunga na CCM.

Madiwani wengine waliotanguliwa na Kimaro katika mfululizo wa maamuzi kama hayo ni Yohana Laiza( Kata ya Kia), Everest Kimathi(Kata ya Mnadani), Abdalla Chiliwi (Kata ya Weruweru), Goodluck  Kimaro (Kata ya Machame Magharibi) na Robsoni Kimaro( Kata ya Uroki).

Ikumbukwe katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 , Chadema kilipata madiwani katika kata zote 17 za Jimbo la Hai.

Madiwani hao wamejiuzulu kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali.

Diwani wa hivi karibuni kabisa kujiuzulu kabla ya Kimaro ni Yohana Laiza ambaye alichukua uamuzi huo kwa sababu ya kile alichokisema kuwa anaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli.

Laiza ambaye alitangaza uamuzi wake huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Sanya Station na kuhudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya , alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kuridhishwa na uamuzi wa mkuu  huyo wa Wilaya ambaye ni mpya,  kutembelea kata hiyo na kusikiliza kero za wananchi hususani mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa Kiwanja cha Ndege cha KIA

Kujiuzulu kwake kulikuja baada ya Agosti 1  mwaka huu, kufikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo, na kusomewa maelezo ya awali ya makosa mawili ya tuhuma za kumbaka na kumsababishia  ujauzito mwanafunzi wa  darasa la saba shule msingi ya Obrien.

Mwendesha mashitaka  mkaguzi  polisi, Hawa Hamisi, mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Devotha Msofe alidai  kuwa upande wa mashitaka umejiandaa kuleta mashahidi kumi kwa ajili ya shauri hilo linalotarajiwa kuanza kusikilizwa Agosti 29 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles