28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

KOFFI ANAN AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 80


Bern, Uswisi

Aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa (UN), Koffi Anan ameaga dunia mapema leo asubuhi leo akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi, Taasisi yake imethibitisha kupitia ukurasa wao wa Twitter.

 

Annan alikuwa Mwafrika wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  alizaliwa mwaka 1938 huko Kumasi nchini Ghana, aliitumikia  UN kwa mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006 na aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel.

 

“Ni huzuni kubwa kuwa familia ya Annan na Taasisi yake ya ‘Koffi Anann Foundation’ kutangaza kuwa aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Koffi Anan amefariki dunia leo Agosti 18, baada ya kuugua kwa muda mfupi,” imeandika  Taasisi ya Kofi Annan.

 

Annan ameacha mke na watoto watatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,491FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles