24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ng’ombe 305,640 kupatiwa chanjo Maswa

Na Samwel Mwanga,Maswa

Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu inatarajia kutoa Chanjo ya Magonjwa ya  Mapele ya Ngozi(LuphySkin Disease)kwa ng’ombe wapatao 305,640.

Pia wilaya hiyo inatatajia kutoa Chanjo ya ugonjwa wa Kuderi kwa kuku asilia wapatao 1,495,216 na Chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa kwa Mbwa wapatao 12,576.

Hayo yameelezwa na Daktari wa Mifugo katika halmashauri ya wilaya ya hiyo, Dk. James Kawamala wakati akisoma taarifa fupi ya zoezi la utoaji chanjo ya mifugo wilayani humo kwa Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge kwenye kijiji cha Senani.

Amesema kuwa Chanjo hiyo inafanyika katika vijiji vyote wilayani humo angalau asilimia 80 ya wanyama hai wanapaswa kupatiwa Chanjo ili kukidhi vigezo vya kitaalam katika udhibiti magonjwa kwa mujibu wa kanuni ya Chanjo na uchanjaji ya mwaka 2020.

Amesema kuwa bei elekezi ya serikali ya Chanjo hizo ni Sh 600 kwa ng’ombe mmoja Sh 2,000 kwa Mbwa mmoja na Sh 100 kwa kuku mmoja.

Naye Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge ambaye ndiye aliyezindua zoezi hilo la uchanjaji kiwilaya lililofanyika katika kijijini hicho amewaagiza viongozi wote kuanzia wilayani humo kuanzia ngazi ya kijiji hadi Kata kuhakikisha mifugo yote katika maeneo yao inapatiwa Chanjo hizo.

Katika zoezi hilo limeshuhudiwa na Wakuu wa idara za halmashauri ya wilaya ya Maswa,Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani humo  pamoja na Sister, Dk. Rosamystica Sambu ambaye ni Afisa Mfawidhi Kanda ya Ziwa,Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles