25.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 31, 2023

Contact us: [email protected]

Neymar azua hofu PSG

PARIS, UFARANSAMSHAMBULIAJI wa Paris Saint Germain, Neymar Jr, amezua hofu huenda maumivu ya nyonga aliyopata katika mchezo dhidi ya Bordeux yatamweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Mbrazil huyo aliumia juzi akiwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa dhidi ya Bordeux na kulazimika kutolewa nje ya uwanja dakika ya 58 na nafasi yake kuchukuliwa na Eric Choupo-Moting.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao PSG ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 licha ya kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Neymar ndiye aliyeifungia PSG bao la kwanza katika kipindi cha kwanza  kabla ya kupata maumivu ya nyonga wakati zikisalia dakika 30 mchezo kumalizika.

Kabla ya mchezo huo nyota huyo pia aliwahi kupumzishwa dakika ya sita katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wakati Brazil ikicheza dhidi ya Cameroon wiki mbili zilizopita jijini London.

Licha ya hali kuwa ya wasiwasi lakini Neymar aliweza kucheza dakika 90 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo, PSG iliifunga Liverpool mabao 2-1 na kuwa nafasi ya pili katika kundi lao ambalo Napoli inaongoza.

Neymar ni mchezaji muhimu wa PSG hadi sasa amefunga mabao 11 katika michezo 12 ya Ligi Kuu Ufaransa msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,315FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles